Ni shetani tu! Mjumbe wa Nyumba 10, Shina Namba 41, Tawi la Viwenge B Majohe, Ilala, Shaibu Selemani Dadi ‘Babu Chinga’ (pichani) amefariki dunia akiwa gesti iliyopo Mjikumbe hukohuko Majohe, Uwazi limefuatilia.
Mhudumu wa gesti hiyo akionesha kitanda alicholalia marehemu siku ya kifo chake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kifo hicho kilitokea Mei 9, mwaka huu ambapo mjumbe huyo aliingia kwenye gesti hiyo na binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22.
Awali, kwa mujibu wa chanzo hicho, marehemu alionekana akipita nyumba hadi nyumba na daftari akichangisha pesa za rambirambi za msiba wa jirani yake.
Awali, kwa mujibu wa chanzo hicho, marehemu alionekana akipita nyumba hadi nyumba na daftari akichangisha pesa za rambirambi za msiba wa jirani yake.
MTOTO WA MAREHEMU AZUNGUMZA
Akizungumza na gazeti hili kwa masikitiko nyumbani hapo, mtoto mkubwa wa marehemu, Zuberi Shaibu alisema yeye ni mkazi wa Keko, Dar, siku hiyo alipigiwa simu na mtu na kuelezwa kuwa, baba yake amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Kaka wa marehemu.
“Hizi taarifa zilinishtua sana, ila sikuwa na jinsi. Na mimi nikampigia simu mdogo wangu na kumwambia twende haraka nyumbani, baba amefariki dunia, lakini kumbe na yeye alishajulishwa juu ya kifo hicho.
“Tulipofika tuliulizia mazingira ya kifo chenyewe, tukaambiwa kuwa, baba yetu alikutwa katika gesti hiyo akiwa amefariki dunia na kwamba alikuwa na msichana ambaye alikimbia.”
“Tulipofika tuliulizia mazingira ya kifo chenyewe, tukaambiwa kuwa, baba yetu alikutwa katika gesti hiyo akiwa amefariki dunia na kwamba alikuwa na msichana ambaye alikimbia.”
BINTI ALIFUNGA MLANGO KWA NJE
“Kibaya zaidi tuliambiwa kuwa, huyo binti aliyekuwa naye chumbani alipoona baba amefariki, alifunga mlango kwa nje kisha akakimbia na funguo. Kwa kweli sisi kama familia, tumehuzunika sana.”
MKE WA MAREHEMU ANENA
Pili Selemani ni mke wa marehemu, yeye alipozungumza na gazeti hili kuhusu kifo cha mume wake, alikuwa na haya ya kusema:
“Siku hiyo mume wangu alifika nyumbani majira ya mchana, akaniachia daftari la michango ya rambirambi, akaniambia anaondoka kidogo kwenda kwenye mambo yake atarudi baadaye.

“Basi, ilipofika jioni nikiwa ndani nimejipumzisha ghafla nilisikia mlango ukigongwa, nikaenda kufungua na kuwaona polisi. Waliniuliza kama mimi ni mke wa Babu Chinga, nikawaambia ndiyo ni mimi.
“Wakaniuliza alipo mume wangu, nikawaambia sijui, wakaniuliza kama hapa kuna ndugu wa karibu mtu mzima, nikawaambia hawapo, wakaenda pembeni, wakaongea jambo huku mimi nikiwa na wasiwasi.
“Baadaye wakanifuata, wakaniuliza kama kuna rafiki wa karibu wa mume wangu, nikawaelekeza, wakamuita, wakaongea naye pembeni kisha wakaniambia nivae vizuri tuondoke. Niliingia ndani kuvaa, tukapanda lile ‘Difenda’ mpaka gesti. Walitangulia kuingia ndani na yule jirani kisha nikaingia na mimi, nikamkuta mume wangu amelala kitandani, wakasema amekufa.” (akaanza kulia).

UWAZI MPAKA GESTI
Uwazi halikuishia hapo, lilikwenda mpaka Mjikumbe ilipo gesti hiyo na kukutana na mmiliki wake, Magambo Rashidi na mhudumu Saidi Almasi ambaye aliwahudumia wawili hao walipofika kuchukua chumba.
Uwazi halikuishia hapo, lilikwenda mpaka Mjikumbe ilipo gesti hiyo na kukutana na mmiliki wake, Magambo Rashidi na mhudumu Saidi Almasi ambaye aliwahudumia wawili hao walipofika kuchukua chumba.
Mmiliki huyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, marehemu alikuwa rafiki yake kipenzi na kifo chake katika nyumba yake hiyo kimemsikitisha sana.
“Hii gesti bado sijaifungua rasmi. Marehemu alipofika alimuona huyu kijana wangu (Saidi) na akampa chumba, akaingia faragha kwa muda. Lakini muda ukazidi kwenda, kijana wangu akaenda kuwagongea, akaona kimya, akagonga sana hakupata jibu.
“Alipoona hivyo na mlango umefungwa kwa funguo, akaenda kuchungulia dirishani, akamuona mzee amelala akiwa mtupu, akamuita sana kimya, ndipo akanipigia simu mimi nikiwa mjini. Nikapitia Kituo cha Polisi Sitakishari, nikaja nao hapa,” alisema mmiliki huyo.
ALIYETOA CHUMBA AANIKA
Naye mhudumu huyo alisema kuwa, marehemu alifika hapo mchana akiwa na msichana mbichi kabisa mwenye umri wa kama miaka 22, akawapa chumba kwa ajili ya matumizi ya muda mfupi.
Naye mhudumu huyo alisema kuwa, marehemu alifika hapo mchana akiwa na msichana mbichi kabisa mwenye umri wa kama miaka 22, akawapa chumba kwa ajili ya matumizi ya muda mfupi.
“Alikuja akaniambia anataka chumba nikamuonesha hiki, akaingia kulala. Ilipofika saa kumi na mbili jioni nikaamua kugonga maana muda ulipita sana. Nilipogonga nikaona kimya, nikachungulia dirishani nikamuona mzee amelala, hana nguo, nikaita hakuitika lakini yule msichana sikumuona. Ni msichana mng’avu. Alipoondoka alifunga mlango na funguo akachukua. Ndipo nikampigia simu mzee,” alisema Saidi.
Marehemu Selemani alizikwa Jumatano ya Mei 11, mwaka huu kwenye Makaburi ya Majohe, Dar.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii