Tuesday, May 17, 2016

Barakah Da Prince ampeleka Kiba Sauz

bara.........Barakah Da Prince
Stori: Boniphace Ngumije
MKALI katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’ amefunguka kuwa kati ya wasanii anaowakubali Bongo, wa kwanza ni Ali Kiba ambaye pia kwa muda mrefu alikuwa akiwaza kufanya naye kazi.
.Ali-Kibaaaaaaaaaa-333Ali Kiba
Akichonga na Uwazi Showbiz, Barakah alisema anamkubali Kiba kwa sababu ni mtu anayeuelewa muziki vizuri na hivi karibuni amemtafuta na kufanya naye kolabo kwa Produza Imma Ze Boy ya Wimbo uitwao Nisamehe ambao video yake wameifanyia Afrika Kusini ‘Sauzi’.
“Ukweli ni kwamba Ali Kiba namkubali sana ni kati ya wasanii ambao mimi ni mshabiki wake, tumefanya kolabo ambayo tunategemea kuiachia soon, watu wategemee kitu kizuri sana kutoka kwangu,” alisema Barakah Da Prince.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta