Sunday, August 7, 2016

BREAKING NEWSS::UGANDA YANUNUA MTAMBO WA KUZUIA KUANGALIA VIDEO ZA UTUPU MTANDAONI,WANANCHI WAMJIA JUU

Yoweri Museveni Rais wa Uganda
Uganda imewekeza kiasi cha dola zakimarekani $88000 katika kununua kifaa hicho na habari hizo zimeishitua sana mitandao ya kijamii.Mashine hiyo ambayo ilinunuliwa kwenya kampuni moja huko nchini Korea ya kusini.

Mashine hiyo inatarajiwa kufika nchini humo mwezi ujao,na utasaidia sana kwa kiasi kikubwa sana mapambano dhidi ya kuangalia video za utupu mitandaoni.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vinadai kuwa waziri wa maadili bwana Fr Simon Lokodo alisema kuwa mashine hizo zitakuwa na uwezo wa kugundua,kukontrol na kuchuja kwa umakini mkubwa sana uwepo wa video na picha za utupu mtandaoni katika vifaa vyote vya kielektroniki.

SOMA PIA::[VIDEO]TAZAMA VIDEO YA MAMA ALIYEJIFUNGUA MAPACHA 4 LIVE KABISA,TAZAMA VIDEO HAPA CHINI NIMEKUWEKEA.
Waziri wa maadili aliongeza na kudai kwamba serikali imetenga kiasi kikubwa sana cha pesa kwa ajili ya kushughulikia  uangaliaji wa video za utupu mtandaoni na wamekaribia kutunga sheria kabisa ya kuweza kupinga swala hilo.

Uangaliaji wa picha za utupu nchini Uganda ni kosa lakisheria na mtu yeyote ambaye atagundulika ana tengeneza mikanda ya ngono na kuisambaza au kuiweka kwenye mitandao ya kijamii anaweza akafungwa mpaka miaka 10 jela.

Uamuzi wa kununua mtambo wa kuzuia video za utupu mtandaoni umepingwa kwa kiasi kikubwa sana na mitandao mingi ya kijamii nchini humo wakidai kuwa serikali imetumia pesa kufanya mambo ambayo hayana maana kabisa.
SOMA BAADHI  YA KOMMENTI  WALIZO ZITOA WATU WA UGANDA KUHUSU SWALA HILO HAPO CHINI

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta