Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa Bingwa wa Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa 29 dhidi ya Ndanda FC uwanja waTaifa Dar es Salaam, licha ya kuwa Yanga tumezoea kumuona Taifa kama mwenyeji ila leo yeye ndio alikuwa mgeni wa Ndanda FC ambao walikubali kuchezea Taifa kama uwanja wa nyumbani.
Katika mchezo huo wa kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu kwa kutetea taji hilo mara mbili mfululizo, wamelazimishwa sare ya goli 2-2, Ndanda FC ndio walianza kufunga goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 28 kupitia kwa Omary Mponda.
Yanga walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 36 kupitia kwa Simon Msuva, lakini dakika ya 40 Donald Ngoma akapachika goli la pili kwa Yanga na kuwafanya Yangakuwa mbele kwa goli 2-1, Yanga waliendelea kuutawala mchezo katika uwanja ambao umejaa mashabiki wake ambao wanasubiria kuona Kombe likabidhiwa, kujisahau kwaYanga kuliwafanya Ndanda FC kuchomoa goli dakika ya 80 kupitia kwa Atupele Green.
A
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii