ILIKUWAJE?
Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.
WAKATUNA BOKO
Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha.
MSIKIE MWENYEWE!
“Mimi naitwa Jerry Kato, nakumbuka mwaka 1982, nilikutana na huyu Sanura (Mama Diamond) pale Mbowe Hotel (sasa Bilicanas iliyopo Posta jijini Dar). Alikuja na jamaa mmoja anaitwa Spencer wakati mimi nafanya kazi ya U-DJ pale, tukatokea kupendana na kuanzisha uhusiano.
“Baada ya muda mrefu, Sanura alinasa ujauzito wakati huo mimi nakaa palepale Mbowe Hoteli, yeye anakaa Saigon (Kariakoo, Dar). Basi akawa anakuja pale hotelini na kunisumbua, si unajua tena mambo ya mimba.
….“Akaniambia alikuwa ananitafuta lakini aliambiwa nimekufa. Basi tukapanga tuonane, akaniambia niende mpaka Sinza (Mori) pale Big Bon, nikifika pale nimpigie simu atanifuata.
…..“Mara akaanza mazungumzo na kuniambia, ‘Jerry unakumbuka?’ nikamwambia nakumbuka, basi akaniambia, ‘sasa leo nataka nikuoneshe mtoto wako’. Akaita Esmaaa…, yule binti akaitika, akaja, akaita tena Nasibuuu, ndiyo akatokea Diamond…”.
“Hapo ndiyo akafanya utambulisho kwa Esma na kumwambia mimi ndiye baba yake hivyo asimsumbue tena. Na kweli nilipomtazama (Esma) anafanana na mama yangu mzazi hata rangi. Ikawa ni furaha tukakumbatiana na maisha yakaendelea.
Chanzo :Global Publishers
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii