Baada ya kuachana na mshiriki mwenzake wa Big Brother Africa, Mbotswana, O’neal, Feza Kessy amesema amelifungua pendo kwa mtu mwingine.
Ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa amejifunza kutouweka uhusiano wake hadharani kama mwanzo.
“Nimemove on, nimekuwa single kwa muda mrefu sasa hivi I am dating, but I am dating mtu ambaye siwezi kumtaja sababu nimejua hiyo biashara ya kuweka watu on public, hapana. I just can’t publicise the person kwasababu ni stress,” amesema Feza.
“Nimejifunza mengi, with me and O’neal kitu ambacho kilinikera, tayari ndio tumeachana na kila mtu alikuwa ana go through process ya kuumia lakini watu wameconcentrate kwenye Oneza, hawajaconcentrate kwamba O’neal ni mtu ambaye anafanya kazi fulani, Feza is an artist, a singer nini they don’t care they just want O’neal and Feza. Kwahiyo hiyo ilinirudisha nyuma,” ameongeza Feza.
Mtazame akielezea hilo na mengine.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii