Msanii wa filamu, Aunt Ezekiel na mpenzi wake Mose Iyobo pamoja na mtoto wao ‘Cookie’, wapo kwenye mchakato wa kuandaa filamu ya fimilia.
Mose Iyobo ambaye pia ni dancer wa Diamond, ameiambia Bongo5 kuwa tayari wapo kwenye mchakato wa kauandaa kazi hiyo.
“Kuna kazi za filamu zinakuja, mtaziona tu, tena familia yetu yote mtaiyona,” alisema Mose. “Unajua Cookie yupo kwenye mikono ya Mama muigizaji na Baba dancer, kwa hiyo ingawa mwenyewe anaweza kuchagua kwa kwenda lakini sisi ndiyo taa yake, kwa hiyo mambo yakikaa sawa mtamuona, Cookie, Baba yake na Mama yake kwenye filamu moja,” alisema Mose.
Pia Mose alisema mtoto wao ‘Cookie’ ataonyeshwa kwa mara ya kwanza hadharani tarehe 21 mwezi huu baada ya kutimiza mwaka mmoja.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii