Muziki wa Singeli umekuepo kwa kipindi kirefu lakini design kama wabongo tulio wengi tumeanza kuuelewa kupitia waimbaji watu kama Man Fongo na Sholo Mwamba.
ManFongo ni mshikaji ambae anazidi kujitengenezea Fanbase hasa kupitia shows za Fiesta ambazo zinaendelea mikoani.
Mkali huyo wa Ngoma ya "Hainaga Ushemeji" amejikuta akiingia kwenye bifu zito na mama wa mrembo Wema Sepetu baada ya kuongea kile kilichotajwa kuwa hakimuhusu huku mpinzani wake Sholo Mwamba akitajwa kuwa chanzo cha beef hilo.
Ubuyu uliozagaa unadai kuwa ManFongo aliongea vibaya kuhusu Mama Wema kilichopelekea Mam huyo kutokwa na povu lisilo la polepole.
GossipCop Soudy Brown hakusita kuwatafuta wawili hao ili watuweke sawa.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii
