Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari, amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Risasi Jumamosi limepewa mchapo.
PICHA ZADHIHIRISHA
Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku wamevaa mavazi ya kulalia (angalia picha Uk. 1).
Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.

Pozi tata
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilicho karibu na Dimpoz, kimepenyeza habari kuwa, licha ya Wema kupitia uhusiano tofauti, Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa kutangazatangaza mambo yake na ndiyo maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya hadi kumuimba kwenye wimbo wake,” kilisema chanzo.

MAZINGIRA YA TUKIO
Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi wetu.
“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

AKUMBUSHIA BIFU LA DIAMOND
Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, kutokana na Diamond kufahamu kuwa, wawili hao wanaendeleza uhusiano, ndiyo maana tangu picha zao za awali zilipovuja mwaka jana wakiwa nchini Afrika Kusini, Diamond na Dimpoz haziivi na hata uswahiba haupo tena kama zamani zile.
“Diamond hataki hata kumsikia Dimpoz katika maisha yake, anamuona ni mtu ambaye hakufanya uungwana kuwa na mtu ambaye yeye tayari ameshatembea naye,” kilisema chanzo hicho.

WEMA ASAKWA
Baada ya kupata ubuyu huo, mwanahabari wetu ‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia anazungumziaje picha hizo na uhusiano huo unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja alisema huenda hakupokea kwa kuwa siku hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.
“Jana (Jumatano) aliniaga ana safari ya Dodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani na wenzake na pengine kelele za wasanii ndani ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.

DIMPOZ HUYU HAPA
Baada ya kumkosa Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.
“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua, Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna kitu kingine zaidi ya ushikaji. Kuna mtu itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema Dimpoz.

KUMBUKUMBU
Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana walipokuwa wakirekodi video ya Ommy, Wanjera nchini Afrika Kusini.
Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa katika vyombo vya habari.
Baada ya hapo, Wema aliripotiwa kutembea na wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan, mshindi wa Shindano la Big Brother Africa-Hot Shot (2014).

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii