March 31 2016 millardayo.com ilipata kibali cha kupiga picha ujenzi unaoendelea wa kupanua uwanja na kujenga jengo jipya kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam, naambiwa huu uwanja unategemewa kukamilika December 2017 na sasa hivi ujenzi wa umekamilika kwa asilimia 60, uniachie na comment yako hapa chini baada ya kutazama hizi picha mtu wa nguvu
Huu ni muonekano wake wa nje kwa sasa ujenzi ukiwa unaendelea
Ujenzi ukikamilika 2017 huu ndio utakuwa muonekano wake wa nje
Muonekano wake kwa karibu sehemu watakapokuwa wanaingilia abiria wanaosafiri
Ujenzi ukikamilika 2017 huu ndio utakuwa muonekano wake wa nje
Hii ni sehemu watakapokuwa wanakaa abiria, ujenzi unaendelea.
Ujenzi ukikamilika patakuwa hivi sehemu wanapopumzikia abiria
Uwanja mpya pia utakuwa na ngazi za umeme na za kawaida ujenzi ukikamilika
Kutakuwa kuna madaraja ambapo ndege inaegeshwa halafu abiria wanashuka au kupanda moja kwa moja na sio kushuka kwenye ngazi zinazobebwa na magari kama zamani
Hili ndio daraja ambapo ndege mbili zinaweza kupark ubavuni kwa mara moja kupandisha abiria au kushusha.
Muonekano wa daraja hilo kwa ndani, abiria akiwa anasubiria kuelekea kwenye ndege.
Ujenzi ukikamilika huu ndio utakuwa muonekano wa uwanja huo kwa juu