Sunday, May 15, 2016

Madee Akanusha Kufumaniwa Akiwa na Shilole Chumbani Wakiwa Watupu

Msanii wa muzuki wa bongo fleva Nuh Mziwanda ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Shilole alisema kuwa aliumia alipomfumania Madee na mpenzi wake huyo wa zamani katika sehemu ambayo si ya wazi yaani chumbani.

Lakini Madee kupitia kipindi cha Planet bongo amekana tuhuma hizo na kusema kuwa suala hilo halina ukweli wowote ule na kudai kuwa Shilole ni rafiki yake ambaye mara kadhaa walikuwa wakitembeleana kwa ajili ya kusalimiana na kupanga mipango mingine ila hakuwahi kutoka na naye kimapenzi na wala hajawahi kufumaniwa na Nuh Mziwanda kama ambavyo inasemekana.

” Siyo kweli Shilole ni rafiki yangu kama marafiki wengine, labda huyo Nuh Mziwanda angeleza vizuri aliwahi kunifumania wapi, lini na wakati gani labda naweza kukumbuka lakini ukweli ni kwamba yule na rafiki yangu kama walivyo rafiki wengine hivyo naomba ieleweke hivyo” alisema Madee

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta