MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, amefunguka kuwa sababu kubwa iliyochangia kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ni kutokana na wanachama wa timu hiyo kushindwa kulipia michango yao ya uanachama.
Simba wamekosa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa nne mfululizo, ambapo mara ya mwisho kuchukua taji hilo ilikuwa ni msimu wa 2011/2012.
“Wanachama wamekuwa wanatupa presha tu wakati wote kuwa timu haifanyi vizuri lakini wao wenyewe wakiambiwa walipe michango hawatoi, sasa wanataka tufanye kitu gani ili timu ifanye vizuri? Usajili tutafanya kutokana na wachezaji ambao tunaendelea kuwatafuta.
“Wengi wao wamekuwa wakijitokeza kwa kulipia kadi zao wakati wa uchaguzi tu unapokuwa umefika, tena hata pesa zenyewe wanakuwa wanalipiwa na watu ambao wanataka kuchaguliwa, hazitoki mifukoni halafu wao ndiyo wanakuwa wa kwanza kulalamika timu mbovu, basi wachangie siyo kulalamika bila mpango,” alisema Poppe.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii