Saturday, May 14, 2016

Giggy Money: Gardner Kwangu Hachomoki

gadner&gigy
Stori: Gift Stanford ‘Giggy Money’ katika pozi na mtangazaji maarufu Bongo wa Kituo cha Redio cha Clouds FM, Gardner G. Habash.
Boniphace Ngumije Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo anayeuza maneno katika Kituo cha Redio cha Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita, Risasi Jumamosi  linakumwagia ubuyu wote.
Akichonga na gazeti hili baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.
“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.
Gazeti hili lilimtafuta pia Gardner ili aweze kufungukia ubuyu huo, alipopatikana alisema;
“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,” alisema Gardner.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta