Mbunge wa zamani wa Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI), David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima
Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuendeshwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
Katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii