Taasisi ya afya ya kimarekani (NIH) imetangaza kufanyika kwa majaribio ya chanjo mpya ya ukimwi nchini Afrika Kusini chini ya njia yake mpya inayoitwa HVTN 702,kupitia chanjo inayofahamika kwa jina la PILOT ACQUIRED IMMUNE DEFICIENCY SYNDROME VACCINE,chanjo inayoonekana kuwa na mafanikio zaidi kuliko chanjo nyingine zote zilizowahi kugundulika.
Katika taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo,wamedai kuwa”Kwa mara ya kwanza katika miaka saba, jamii ya wanasayansi imekua katika majaribio makubwa ya chanjo ya kukabiliana na Virusi vya Ukimwi (VVU),na kufanikiwa kupatikana kwa chanjo hii,ikiwa ni matunda ya miaka mingi ya utafiti na majaribio,” alisema Dk Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Allergy na Magonjwa ya kuambukiza (NIAID), ambayo ni sehemu ya Taasisi ya N.I.H.
Majaribio ya chanjo hiyo yataanza kufanyika mwezi November katika majiji 15 nchini Afrika Kusini,hii ikiwa ni baada ya chanjo hiyo kutibu asilimia 34 ya watu walipewa chanjo hiyo nchini Thailand mwaka 2009,ambapo katika majaribio ya chanjo hii nchini Africa kusini,taasisi hiyo imepanga kuwapa chanjo hiyo zaidi ya watu 5,400 wanaume kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 hasa wale walio kwenye mazingira hatarishi ya kupata virusi vya ukimwi,huku majibu rasmi ya matokea ya chanjo hiyo yakitarajiwa kutoka mwaka 2020.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii