Wednesday, May 18, 2016

Askofu, mkewe wazua timbwili kanisani

kANISANI (1)Timbwili kanisani.  
DAR ES SALAAM: Timbwili! Waumini wa Kanisa la Heaven of Peace Christian Church lililopo Ubungo Kibangu jijini hapa, Jumapili iliyopita walishindwa kuendelea na ibada baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na wake wawili wa Askofu wa kanisa hilo, Alphonce Lubalati, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo eneo la tukio.
Asubuhi ya siku hiyo, chanzo chetu kilitonya kuhusu harufu ya timbwili kanisani hapo ambapo bila kupoteza muda, waandishi wetu wakiwa na vitendea kazi vyote, walitinga eneo la tukio na kunasa tukio zima, mwanzo hadi mwisho.
TIMBWILI LILIVYOANZA
Kama ilivyo kawaida ya Jumapili, waumini wa madhehebu ya Kikristo hujumika kwa ajili ya ibada ambapo waumini wa kanisa hilo lililopo Mtaa wa jeshini, Ubungo Kibangu, nao walianza kuwasili kanisani hapo, mmoja baada ya mwingine.
kANISANI (3)Miongoni mwa waliowasili, alikuwemo Teopister Aloyce ambaye inadaiwa kuwa ni mke wa askofu huyo ambaye aliwasili akiwa ameongozana na mchungaji mpya wa kanisa hilo, Augustino Nyanyaro.
Baada ya mwanamke huyo kuwasili, minong’ono ya chini kwa chini ilianza na baadaye, vijana waliojitambulisha kama watoto wa askofu huyo aliowazaa kwa anayedaiwa kuwa mke mkubwa (jina lake halikupatikana mara moja) ambao walikuwa miongoni mwa waumini, walisimama na kuanza kufanya fujo.
kANISANI (2)MADAI YALIVYOKUWA
Vijana hao, walikuwa wakipaza sauti wakimtaka mwanamke huyo (mke mdogo- Teopistar) aondoke kanisani hapo kwa sababu yeye ndiyo chanzo cha baba yao kuwatelekeza na kwenda kuishi naye Tegeta, nje kidogo ya jijini Dar.
Baadhi ya waumini walilazimika kutimua mbio kuokoa nafsi zao kwani kwa hali ilivyokuwa, kulikuwa na uwezekano wa kutokea vurugu kubwa zaidi.
kANISANI (6)Askofu akiondoka eneo la tukio.
MKE MKUBWA AIBUKA
Wakati vurugu hizo zikiendelea, mwanamke anayetajwa kuwa ndiyo mke mkubwa, ambaye anaishi ndani ya eneo lilipo kanisa hilo, naye aliibuka na kuungana na wanaye, wakamvaa mwanamke huyo wakimtaka aondoke eneo hilo.
Mshikemshike ukaendelea huku Askofu Lubalati na Mchungaji Nyanyaro wakijitahidi kutuliza hali ya mambo bila mafanikio.
kANISANI (7)Askofu wa kanisa hilo akiingia kwenye gari aondoke.
MJUMBE AINGILIA KATI
Vurugu hizo zilizovuta hisia za wengi, zilimfanya mjumbe wa mtaa huo, Juma Mgata kuingilia kati na kumsihi mke mkubwa na wanaye, wasubiri ibada iishe ndipo wakae chini na kulishughulikia tatizo hilo.
Walitulia kwa muda lakini baadaye uzalendo uliwashinda, wakakinukisha tena, safari hii wakiwadunda hadi waumini waliokuwa wakimtetea mke mdogo.
Muumini mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa watoto hao pamoja na ndugu wengine kwa madai kwamba katika vurugu hizo, alimpiga kibao mke mkubwa.
WATOTO WANASEMAJE?
Watoto wa askofu huyo waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walisema Teopister alikuwa mtumishi kanisani kwa baba yao lakini baadaye walianzisha uhusiano wa kimapenzi na hatimaye kuoana, na kusababisha baba yao awatelekeze kwa kutowapelekea mahitaji muhimu, ikiwa ni pamoja na kuhama kabisa nyumbani kwenda kuishi na mwanamke huyo.
“Huyo mwanamke ameona sisi tunavyopata shida kwa kukosa msaada wa baba haitoshi, leo anakuja kusali hapahapa nyumbani kwetu, ni haki kweli?” alisema mmoja wao.
kANISANI (5)Msikie askofu
Alipotafutwa Alphonce Lubalati kuzungumzia tukio hilo, alisema kwa muda huu (saa 11.00 jioni) Jumatatu, yupo serikali za mtaa alikoitwa kuhusiana na shauri hilohilo, hivyo akaomba aachwe.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta